
- Kwa asili yake mwanadamu ni roho na roho hiyo imepewa nyama na mifupa na kuonekana katika namna ya mwili. Muungano kati ya mwanamke na mwanaume katika kuzaa mtoto ni tendo takatifu na la kiungu kwakua roho mbili zilizovalishwa mwili zinaungana kuumba mwanadamu mmoja mwenye roho kamili. Katika mchakato huu mwanamke ndio ufunguo wa udhihirisho wa uumbaji unaozalisha maisha ya mwili mpya wenye roho kamili. Mwanamke ni nguzo kwenye malango yanayoingia mjini.
- Anga la kiroho linajengwa katika via vya usazi vya Mwanamke, humo yale yaliyofichika katika ulimwengu wa roho yanawekwa wazi kwa namna ya mwili unaojengwa tumboni mwa mama. Wanawake ni miungu kwakua ndio wanaofanya uhai wa mwanadamu kwa kubadilisha maji na damu kuwa mifupa na nyama, vinavyomfanya mtu.
- Mungu ametumia mwezi kama alama ya kiroho ya majira na nyakati. Mwanamke sio mwili wa nyama tu bali ni chombo cha kiroho. Hii inadhihirishwa tukiangalia mzunguko wake wa hedhi ambapo hautegemei kalenda zilizowekwa kwa utashi wa kibinadamu bali huongozwa na mzunguko wa mwezi na nyota mbinguni. Nguvu za kiroho za mbinguni zinadhihishwa kwakutumia mwili dhaifu wa mwamke.
- Mwanaume ni wa mwilini na mwanamke ni wakiroho, ufahamu huu ndio utajenga utangamano na utulivu katika maisha ya mwanadamu. Mwanaume anashiriki nguvu za uumbaji pale mwanamke anaporuhusu aingie malangoni mwake kushuhudia ulimwengu wa kiroho uliomo ndani yake huyo mwanamke.
- Mwanaume anapotaka kujiona yeye mwenyewe ni lazima aingie katika mji wa mwanamke kuptia malango yake na apande mbegu yake humo. Mwanamke katika maji ya uhai anakua chombo cha kumjenga mtu kwakutumia vinasaba(DNA) kwenye shahawa, kama taarifa za kiroho kumuumba mwadamu mume au mke.
- Mwanadamu na ulimwengu nilazima uheshimu sana wanawake kwasababu wao ndio miungu wa Kwanza na dhahiri tunaoweza kumwona hadi pale walipoamua kutujulisha juu ya Mungu muumbaji na mababu. Kwanini wanawake Sasa huwanyonyesha wanaume maziwa na kuwapa watoto maziwa ya kopo? Kama mume wako anataka kunyonya tena Kama mtoto mchanga, mrudisha kwa mama yake.
- Mababu au somo waliotangulia zamani, ni mizizi mama au chimbuko Mudzimu(Shona) Mizimu(Swahili) yaani mudzi-mai, mudzi- mzizi, Mai – mama. Kwakua neno hili linaashiria chimbuko letu ni mwanamke, kumtukana mwanamke ndi sawasawa na kujipalia makaa ya Moto kichwani. Bababu zetu wanajidhihirisha tena na tena kwa kupitia mwanamke.
- Ni laana kwa kijana kulala na mama yake na katazo kumtusi kwa kutaja sehemu za Siri za mama kwani kutamka vibaya kuhusu malango ya mji ni kukosa heshima kwa zawadi ya uhai wanayoleta. Ni ujinga kutukana malango ya mji. Wanawake ni watakatifu na wanaume wote wajue na kuwaheshimu.
- Watoto mliowazaa ni nyinyi wenyewe na ninyi ndio chanzo Cha watoto wenu kwakua kilichopo ndani yenu ndio kimewafanya wao kuwa. Yaliyofichika yamewekwa wazi kwa njia ya muunganiko wa mama na baba.
- Ni Babu na Bibi wakirejea kwa umbo la watoto wenu kutambulisha nasaba zetu tangu kale.
- Waheshimu watoto wako kwani wao ni mababu wa kale usio wakumbuka tena, wako katika mwili mpya ,wamerudi tena kutoka katika mzizi kama ule wa Daudi. Kutoka katika mzizi kila mzazi anajizaa mwenyewe kwa watoto wake.
- Chakula tulacho ambacho huchukua madini na virutubisho kutoka katika udongo huunganisha madini na virutubisho vingine na kuujenga mwili. Mwili wako hubadilisha maumbile hayo ya kisayansi kwa kutumia vinasaba na kuwa mtu hai.Udongo umeunganishwa na Mababu ambao wamekuwa mavumbi tena, wanarudi Tena kwetu kama nguvu ya nishati,mimea tiba na hewa nzuri kutoka msituni.
- Fahamu asili yako, utajua nguvu na udhaifu wa mababu zako na namna inavyoathiri tulivyo. Karama,ujuzi,uwezo wa ufahamu wetu umenakiliwa katika vinasaba vyetu kutoka kwao.
- Kutokana na uwezekano wa kuharibika vinasaba, sio sahihi kuoana ndugu kwani inaweza kusababisha kutokea kuharibika kwa vinasaba na kuzaliwa watoto walemavu.
15.Viungo vya uzazi ni zana za kiroho, zinatumika kuwasiliana kimwili na kiroho Kati ya watu na kujenga muunganiko wa ushirika katika uumbaji.
16.. Mbingu na nguvu zake za kiroho zimewekwa ndani ya tumbo la mwanamke. - Jioshe na ujitakase kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Vua viatu vyako kwani ardhi unayoikanyaga nintakatifu. Kila mwanamke amkumbushe kila anae mariposas katika mji wake juu ya utakatifu wa hekalu lake.
- Ni kosa lisilosameheka kwa mwaume kufanya tendo la ndoa na mwanamke kwa nguvu bila ridhaa yake. Hakuna uzuri Wala fahari ya ukatili wa kingono na ubakaji. Wafundishe watto komba yangu wakiwa wadogo, wafundishe kudhibiti hisia za kukataliwa. Lazima wazoee kusikia na kuheshimu neno HAPANA!
- Mwanaume hutumia udhaifu na nafasi iliyo rahisi kwake lakini mwanamke hufanya maamuzi. Mwamke Ana haki ya kuamua ni mwanaume gani awe na watoto nae.Baafa ya mapendekezo kadhaa atachagua wakushirikiana nae katika wajibu huo mtakatifu.
- Hakuna mwanaume anatakiwa kujisifu kuwa na mke mzuri, ni kwa mwanamke kujisifu kwa chaguo lake sahihi. Mwanamke anaeolewa na mwanaume mwenye hekima anathibitisha kuwa na chaguo zuri.
- Enyi wanawake, Kama mumeo ni msumbufu, yeye sio tatizo, kumbuka Ni chaguo lako na wale wengine uliowaacha hukuwachagua.
- Wanawake ni milango na wanaume ni nyaya za kuunganisha kale, Sasa na kesho.
- Epuka kupanda mbegu mwambani kwakua mzinzi na muasharati atakugeuza kuwa mkate wa kuliwa na kutupa mbali kifungashio chake.
24.Muwe na lugha na maneno yenye baraka miongoni mwenu na mjenge jamii ambayo kila mmoja anafurahia kuishi. - Mwanamke mjinga huongea kwa kupayuka na hafanyi chochote, lakini mwenye hekima hunong’ona busara na subira na hata milima yaweza ondoka kwa bidii zake.
- Maji yaliyo ndani ni lazima yaunganishwe na maji yaliyo nje.
- Udongo wa nje ni lazima uungane na ule wa ndani
- Upepo(roho) wa ndani lazima uungane na wa nje. Hii ni kanuni ya msingi ya ustawi na maisha yenye afya.
- Jipe muda wa kutafakari, kupumzika, kuangalia jua na mwezi, kutembea msituni au ufukweni bila viatu kwani kutoka udongo tulitoka na tutarudi.
- Umba dunia yako kwa kauli yako mwenyewe. FoT